ALAN SHEARER AIVUA UBINGWA LEICESTER CITY MSIMU HUU... asema nafasi ipo kwa timu sita nyingine

NAHODHA wa zamani wa Newcastle na England, Alan Shearer ameivua ubingwa Leicester City akisema haina ubavu wa kutetea taji hilo msimu huu.

Shearer ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka kwenye runinga, anasema anaziona timu zenye ubavu wa kupigania ubingwa kwenye msimu huu ni sita na Leicester haimo katika kundi hilo.

“Mimi sio mtabiri lakini kwa hakika Leicester haina nafasi yoyote ya ubingwa msimu huu, nafasi hiyo ipo Katika timu sita tu ambazo ni Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham,” alisema Shearer.


Mshambuliaji huyo aliyetikisa enzi zake, aliyasema hayo muda mfupi kabla ya pazia la Ligi Kuu England kufunguliwa hapo Jumamosi na Leicester City kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Hull City.

No comments