ALEXANDRE LACAZETTE AWAPA MATUMAINI MASHABIKI WA ARSENAL

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Lyon ambaye amekuwa akifukuziwa na Arsenal kwa muda mrefu, Alexandre Lacazette ameibuka na kutoa kauli ya matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kusema, angejisikia furaha kama angepata nafasi ya kucheza nje ya Ligi Kuu ya Ufaransa.

Mwezi uliopita Arsenal ilijikuta ikikataliwa ofa ya pauni mil 30 iliyopeleka Lyon kwa ajili ya kumnasa Lacazette ingawa imeelezwa kuwa bado wanaisaka saini ya straika huyo.


“Kama kuna ofa yoyote ambayo haiwezekani kukataliwa, sitaikataa,” alisema Lacazette mara baada ya kuifungia timu yake “hat trick” katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nancy.

No comments