ARSENAL MAMBO SI SHWARI, YAOKOTA POINTI MOJA YA KWANZA


ARSENAL bado haijachanganya – hii ni baada ya kumaliza mchezo wa pili wa Premier League bila ushindi.

Klabu hiyo ya London ilanza ligi kwa kukubali kichapo cha 4-2 kutoka kwa Liverpool na leo imeambulia sare tasa dhidi ya Leicester City.

Kwa matokeo hayo, Arsenal tayari imejikuta iko nyuma kwa pointi tano dhidi ya mahasimu wake Manchester United, Manchester City na Chelsea ambazo zote zimeshinda michezo yao miwili ya mwanzo.

Aidha, matokeo hayo pia yanaiweka pabaya Leicester City ambayo ni bingwa mtetezi kufuatia kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Man United.

No comments