Habari

ARSENAL YAKUMBWA NA KIWEWE CHA KUSAKA SENTAHAFU MPYA

on

West Brom have stunned Arsenal by valuing veteran defender Jonny Evans at £25m
KLABU ya Arsenal imeripotiwa kumpigia hesabu beki wa kati wa Atletico
Madrid, Jose Gimenez ili iweze kutatua tatizo lake katika safu ya ulinzi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, tayari makachero wa klabu hiyo ya
The Gunners wapo kwenye mazungumzo na nyota huyo kuona kama wataweza kumpata
kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Jose Gimenez  ni sehemu tu ya
mawindo ya Arsenal ambayo pia inamwania beki wa Valencia Shkodran Mustafi na
beki wa zamani wa Manchester United Jonny Evans.
Arsenal inataka kunasa mmoja kati ya mabeki hao watatu lakini hadi
sasa juhudi zao zinakwamishwa na bei mbaya za nyota hao.
Valencia imesema Mustafi hataondoka bila pauni milioni 42 huku bei ya
Evans  (pichani juu kushoto) ikitajwa kufikia pauni milioni 25.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *