ARSENE WENGE ASEMA MSIMU HUU NDIO UTAKAOAMUA HATMA YAKE NDANI YA ARSENAL

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba hatma yake kwenye klabu hiyo ya Emirates itategemea matokeo ya msimu huu.

Wenger aliyasema hayo juzi katika mahojiano na shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, akisema kwamba mkataba wake utamalizika mwakanai na hivyo atakachokifanya kitategemea matokeo hayo.

“Mkataba wangu utakamilika Juni mwakani, kwahivyo nitakachofanya baada ya hapo itategemea na matokeo ya msimu huu,” alisema Wenger.

Raia huyo wa Ufaransa, 66, aliajiriwa mwezi Septemba, 1996 kuiongoza klabu hiyo.

Mkataba wake wa sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.

Arsenal haijashinda taji la Ligi Kuu Uingereza tangu mwaka 2004, jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger, hasa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.


Awali Wenger alikuwa amehusishwa na wadhifa wa kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua pahala pake Roy Hodgson.

No comments