ARSENE WENGER AJITETEA KUHUSU KUTOSAJILI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kwamba hana mpango wa kupangua kikosi chake na akasema kuwa atafanya hivyo kwa kununua mchezaji wa kuongeza ubora katika timu hiyo.

Kwa mara nyingine Mfaransa huyo amekaliwa kooni kwa kushindwa kusajili wachezaji wengine msimu huu, baada ya kumsajili mchezaji mmoja, Granit Xhaka wakati Ligi haijaanza.

Akizungumza juzi kabla ya mechi yao ya jana dhidi ya Liverpool, Wenger alisema kuwa hakuna haja ya kusajili wachezaji wengine kwa sasa.

“Shinikizo haliwezi kufanya ukashinda mechi,” alisema kocha huyo. “Kinachoweza kufanya ukashinda mechi ni ubora wa kiwango na soka lako, hivyo kinachotakiwavni kuelekeza nguvu katika hilo.”

Alisema kuwa katika soka la kisasa kuna mambo mengi magumu kutokana na kulazimishwa kuwa na wachezaji wapya.


Arsenal ilikuwa ikimfukuzia nyota wa timu ya Lyon, Alexandre Lacazette lakini ofa yao ikapigwa chini na vinara hao wa soka Ligue 1 na alipohojiwa kama atasajili straika mwingine ili kumsaidia Olivier Giroud, Wenger alisema kuwa wana alexis Sanchez na Theo Walcott na hivyo haoni haja ya kuumiza tena kichwa.

No comments