Habari

ARSENE WENGER SASA ROHO KWATU BAADA YA KUMSAJILI LUCAS PEREZ KWA PAUNI MIL 17

on

Perez started his career at Atletico Madrid C before joining neighbouring club Rayo Vallecano
ARSENE WENGER amemmwagia sifa mshambuliaji wake mpya Lucas Perez aliyesajiliwa na Arsenal kutoka Deportivo La Coruna.
Perez alibakia kuwa mshambuliaji pekee aliyekuwa akisakwa na Arsenal katika siku za kuelekea ukingoni mwa  dirisha la usajili la kiangazi na hatimaye  usajili wake ukakamilika Jumanne mchana kwa ada ya pauni milioni 17. 
Kocha huyo wa Arsenal amesema Perez aliyefunga mabao 17 kwenye La Liga msimu uliopita, ni suluhisho tosha la safu yake ya ushambuliaji.

LUCAS PEREZ 

Kuzaliwa: Septemba 10, 1988
Timu: Rayo Vallecano, Karpaty Lviv, PAOK, Deportivo La Coruna, Arsenal
Mechi alizocheza: 178
magoli: 52
“Siyo tu ni mfungaji, bali ni mtu anayeshirikiana vizuri sana na wenzake uwanjani,” Wenger aliiambia tovuti ya Arsenal.
“Ana jicho zuri kwenye goli na alikuwa na msimu bora mwaka uliopita”
Wenger hakuficha furaha yake kwa kumsajili mshambuliaji huyo  baada ya kushuhudia maombi yake ya kuwasajili washambuliaji kadhaa yakipigwa chini na vilabu vyao.

Arsenal have completed the £17million signing of Lucas Perez from Deportivo La Coruna
Arsenal imekamilisha usajili wa Lucas Perez kutoka Deportivo La Coruna
The 27-year-old scored 19 goals in all competitions for Deportivo La Coruna last season
Lucas Perez  mwenye miaka 27 akipozi na ‘uzi’ wa Arsenal

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *