BALOZI WA MAREKANI NCHINI INDIA AMWOMBA RADHI SHAH RUKH KHAN KWA KUMCHOMESHA MAHINDI UWANJA NDEGE

BALOZI wa Marekani nchini India amemuomba radhi staa wa Bollywood, Shah Rukh Khan, kwa kusoteshwa uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport Ijumaa iliyopita.

Khan aliwambia mashabiki wake kupitia mtandao wake wa kijamii kuwa, amefadhaishwa sana kuzuiwa kwa muda mrefu kwenye uwanja huo wa ndege na mamlaka husika bila ya kuambiwa sababu.

Balozi huyo wa Marekani aliomba radhi kwa msanii huyo, ndugu, jamaa na wananchi wote na serikali India ikiahidi kuwa tukio kama hilo halitatokea tena.


Mcheazji huyo wa filamu za kibabe alienda Marekani katika shughuli zake za kikazi ambako alipata mwaliko kutoka kwa wasanii wa Hollywood.

No comments