BRAVO ATUA MAN CITY KUMMALIZA JOE HART ...Guardiola asema aisyetaka na aondoke


Claudio Bravo is set to join City for £17million after arriving in Manchester on Tuesday

HATMAYE klabu ya Barcelona imeridhia ombi la kocha wake wa zamani Pep Guardiola aliyeomba kumchomoa kipa Claudio Bravo - na kilichofuatia baada ya hapo ni kukamilika kwa usajili wa pauni milioni 17.

Bravo alitua England jana kwaajili ya kukamilisha usajili wake huo unaofanya hatma ya kipa namba moja wa England Joe Hart iwe mashakani.

Hadi sasa hivi Hart hajacheza mchezo wowote na ujio huu wa Bravo ni ishara mbaya kwake.

Hart, mwenye miaka 29 raia wa Uingereza aliyeichezea City mechi 347 amepoteza nafasi kwa Willy Caballaro.

Hata hivyo Guardiola kocha aliyeipa Barca mataji mengi zaidi katika historia ya klabu hiyo, amesema bado Joe Hart yupo kwenye mipango yake.

Lakini Guardiola amekuwa na kauli tata juu ya Hart na hivi karibuni alisema: "Joe anaweza kuondoka kama hana furaha. Sitaki kuwa na wachezaji wasio na furaha, wanaweza kuondoka ila wakitaka kubaki basi wabaki na tuipiganie timu pamoja".


Bravo kipa raia wa Chile aliyeidakia Barcelona mechi 75 tangu alipotua mwaka 2014 akitokea Real Seciedad, ametua City kwa lengo moja tu – kuwa kipa wa kwanza – ingawa anajua kuna ushindani mzito.

No comments