BRAZIL NA SWEDEN WANAWAKE DIMBANI KESHO RIO DE JANEIRO

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake wa Brazil, kesho Jumanne itashuka dimbani kusaka tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Olimpiki 2016.

Brazil walijikatia tiketi hiyo kwa kuitoa kwa matuta Australia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo iliyopigwa juzi.

Katika mchezo huo, kipa Barbara ndie aliyeiwezesha Brazil kupata ushindi huo baada ya kupangua penati mbili na kuifanya nchi yake kushinda kwa mikwaju 7-6 dhidi ya Australia.

Ndani ya dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, huku wenyeji Brazil wakiwa kwenye shinikizo la mashabiki wenye wazimu wa soka.

Mikosi ilitaka kuwaandama Brazil tangu mapema kwani staa wao Marta alikosa penati yake na kuamsha presha, lakini Barbara akafuta makosa hayo kwa kuzipangua penati za Katrina Gorry na Alana Kennedy, hivyo kuifanya Brazil kutinga nusu fainali.


Mchezo huo dhidi ya Sweden hapo kesho ni muhimu kwa Marta kupunguza uchungu wa kukosa penati ambapo atatakiwa kutulia na kusaidia nchi yake kutunga fainali, wakati nusu fainali nyingine ni kati ya Canada na Ujerumani.

No comments