Habari

CHELSEA HATARINI KUMKOSA ROMELU LUKAKU

on

Romelu Lukaku had an off-night in front of goal during Everton's 4-0 win over Yeovil
LICHA ya kushindwa kutikisa nyavu katika  mchezo wake wa kwanza msimu huu, bado kocha Ronald Koeman anaamini Romelu Lukaku ndiye atakayekuwa mwiba wa timu pinzani.
Everton iliifumua Yeovil 4-0 kwenye dimba la Goodison Park ikatika raundi ya pili ya EFL Cup (Capital One) kwa magoli ya  Aaron Lennon, Ross Barkley na Arouna Kone aliyetupia mawili.
Lukaku aliyefunga mabao 25 msimu uliopita akashindwa kuliona lango kwenye karamu hiyo ya magoli, ukiwa ni mchezo wake wa kwanza msimu huu. 
Koeman amekataa kukubali uvumi kuwa mshambuliaji huyo akili yake ipo katika uhamisho wa kwenda Chelsea na badala yake amedai Lukaku anaheshimu mkataba wake Everton.
Inaaminika Romelu Lukaku yuko mbioni kupewa mkataba mpya wa kuendelea kukipiga klabuni hapo hali inayotoa picha kuwa hana tena fikra za  kurejea Chelsea.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *