KOCHA Claudio Ranieri ameiponda Leicester City akisema kuwa Hull City ni wazuri kuliko mabingwa hao watetezi wa michuano ya Ligi Kuu England, baada ya kuwachapa kwa mabao 2-1 na huku Muitaliano huyo akiwalalamikia wachezaji wake kwa kukosa nguvu.

Alikuwa ni mchezaji Riyad Mahrez aliyeipa matumaini Leicester City baada ya kusawazisha bao la kwanza lililofungwa na Adama Cromande, lakini Robert Snodgrass akayeyusha kwa kupachika bao la ushindi lililowafanya mabingwa hao kuondoka nyumbani wakiwa mikono mitupu.


“Hull imecheza vizuri,” Ranieri aliliambia Sky Sport. “Tulijaribu kuonyesha ubora wetu, tulifanya baadhi ya makosa hivyo tunatakiwa kutafakari pale tulipokosea.”
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac