Habari

DELLE ALLI AAMUA KUBADILI JINA LA JEZI YAKE KWA SABABU ZA KIFAMILIA

on

Kiungo wa Tottenham Dele Alli atacheza msimu huu kwa kuvaa jezi yenye jina lake la kwanza “Dele” badala ya lile la pili “Alli” alilokuwa akilitumia hapo awali.
Mchezaji huyo anasema kuna sababu zake binafsi na za msingi zilizopekelea hatua hiyo ya kubadilisha jina la kutumika kwenye  jezi yake yenye namba 20.
Kinda huyo wa miaka 20 amesema ajiskia kuwa hana muunganiko na hilo jina. Alli amekuwa akiishi mbali na familia yao tangu akiwa na umri wa miaka 13.
“Nataka jina la jezi yangu liwasilishe vile nilivyo na najiskia sina mahusiano na hilo jina la Alli,” alisema kiungo huyo wa Tottenham.
“Huu ni uamuzi ambao nimeuchukua baada ya kujadiliana na wanandugu wa karibu.”
Mama wa Alli aliachana na mwanae akiwa na umri wa miaka 13 wakati akipambana na matumizi makali ya pombe na kulazimishwa kuwapeleka watoto wake kwenye vituo ya kijamii.
Nyota huyo wa England akalelewa na Alan na Sally Hickford ambao anasema kwa sasa anawaona wawili hao kama wazazi wake.
Tottenham midfielder Dele Alli will wear the name 'Dele' on his shirt this season
Kiungo wa Tottenham Dele Alli sasa atavaa jezi yenye jina ‘Dele’ msimu huu
Alli had previously worn his surname on his shirt but has switched for personal reasons
Alli ameamua kutotumia tena jina la ukoo kwenye jezi yake
The Tottenham midfielder also wore the name 'Alli' at Euro 2016 with England
Kiungo huyu wa England alitumia jina la ‘Alli’ kwenye Euro 2016 akiwa na England

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *