DOGO JANJA ASEMA WIMBO WAKE WA "MY LIFE" UMEMTOA ZAIDI

MSANII wa muziki wa Bongofleva, Dogo Janja amesema kuwa wimbo wake wa “My Life” umempatia mafanikio makubwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, msanii huyo alisema kuwa amepata mafanikio makubwa sana ndani na nje ya Tanzania.


Baada ya wimbo huo kukubalika nchini Kenya, Dogo Janja anasema kuwa anaamini utafanya poa zaidi siku za mbeleni na kumweka katika wakati mzuri kwa mashabiki wake.

No comments