DULLY SYKES ASEMA WIMBO WA "INDE" ALIPANGA KUFANYA NA DIAMOND PLATNUMZ LAKINI ...

DULLY Sykes amedai kuwa awali alipanga kumshirikisha Diamond kwenye wimbo wake mpya wa “Inde” aliofanya na msanii wa WCB, Harmonize.

Akiongea katika kipindi cha 180 Power cha Sibuka FM siku kadhaa zilizopiya, Dully alisema baada ya kuona Diamond yuko bize, ndipo kura yake ikamwangukia Harmonize.

“Huu wimbo kwanza nilipenda kufanya na Diamond,” alisema mwimbaji huyo mkongwe anayefahamika pia kama “Mista Misifa.”

“Lakini nikaona Diamond yuko bize sana nisimsumbue, nikaangalia after Diamond nani anastahili nikaona Harmonize anafaa kati ya vijana niliowafikiria.”

Inde umekuwa wimbo wenye mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi, huku video yake ikiwa na zaidi ya views 500k hadi sasa.

No comments