GONZALO HIGUAIN AWAAMBIA JUVENTUS WAKAE MKAO WA KULA


Gonzalo Higuain wheels away in celebration after scoring Juventus' winner on Saturday

STAA Gonzalo Higuain ametaka mashabiki wa Juventus wakae mkao wa kula na kutegemea makubwa kutoka kwake hususan katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Higuan ambaye ameanza kuthibitisha thamani yake ya euro mil 90 baada ya kuifungia bao lake la kwanza na kuifanya timu yake kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Florentina, amesema anapigana kuiwezesha Juve kutwaa Champions League.

Higuain aliyetua Juve akitokea Napoli, amesema pamoja na kwamba anatamani kuchukua ubingwa wa Italia, lakini anaamini mashabiki wa Juve wana kiu zaidi na ubingwa wa Ulaya.

“Nimefurahi kucheza mchezo wangu wa kwanza kwa ushindi na kufunga bao, mambo mazuri zaidi yako njiani” alisema nyota huyo alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Mediaset Premium.No comments