Habari

IBRAHIMOVIC AENDELEA KUMIMINA RAHA MANCHESTER UNITED …Paul Pogba aonyesha thamani yake

on

The 34-year-old Swede leaps with joy as his 36th-minute header gives United the lead as Old Trafford erupts 
Zlatan Ibrahimovic ameendelea kuwapa raha mashabiki wa Manchester United kwa kufunga mabao yote mawili wakati klabu hiyo inayonolewa na Jose Mourinho ilipoitandika Southampton 2-0 Ijumaa usiku.
Katika mchezo huo mkali wa Premier League, Ibrahimovic alifunga bao moja katika kila kipindi na kufanya afikishe jumla ya mabao matatu kwenye ligi ukijumlisha na lile alilofunga Jumapili iliyopita  United ilipoifunga Leicester City 3-1.
Kama kuna wakati uliovuta hisia za watu wengi ni pale refarii Anthony Taylor alipoamuru penalti baada ya Luke Shaw kuangushwa ndani ya box  ambapo hapo ndipo ilipobainika kuwa nafasi ya nahodha Wayne Rooney kuendelea kuwa mpiga penalti imeyeyuka.
Wakati Rooney akiangalia kwa tabasamu eneo la kupigia penalti, Ibrahimovic akauchukua mpira na kwenda kuuweka eneo husika. Rooney sasa anaishi kwenye ulimwengu wa Zlatan ambao una mtu mmoja tu anayepiga penalti – Zlatan Ibrahimovic.
Mshambuliaji huyo mwenye umbo kubwa akafunga penalti hiyo kwa shuti kali lililokwenda kushoto huku kipa Fraser Forster akiruka kulia.
Paul Pogba aliyesajiliwa kwa pauni milioni 100 kutoka Juventus alicheza mchezo wake wa kwanza kuthibitisha ubora wake kwa namna alivyokuwa akihaha uwanja mzima huku akitoa pasi za uhakika, chenga za kuvutia sambamba na kuhusika na mashambulizi mengi lakini pia akisaidia kudhibiti mashambulizi yaliyoelekezwa kwenye lango la United.
Hakuna ubishi kuwa kiwango cha Pobga kitawapa jeuri kubwa mashabiki wa Manchester United.
MAN UTD (4-2-3-1): De Gea 6; Valencia 6, Bailly 6.5, Blind 6.5, Shaw 7; Pogba 7, Fellaini 6.5; Mata 7 (Mkhitaryan 76, 6), Rooney 6.5 (Smalling 89), Martial 6.5; Ibrahimovic 7.5. 
Subs not used: Young, Rashford, Romero, Herrera, Schneiderlin
Wafungaji: Ibrahimovic 36, 52
SOUTHAMPTON (4-3-1-2): Forster 6.5; Soares 6, Van Dijk 6.5, Fonte 5.5, Targett 6; Hojberg 6.5, Romeu 6 (Clasie 12, 5.5), Davis 5.5 (Austin 67, 6); Tadic 6.5; Long 6.5, Redmond 7.
Zlatan Ibrahimovic rises high to meet Wayne Rooney's superb cross sending a thunderous header towards goal 
Zlatan Ibrahimovic akiruka juu kuunganisha kwa kichwa krosi ya Wayne Rooney na kufunga bao la kwanza
Ibrahimovic and Pogba watch on as the former PSG striker's bullet header heads for the bottom of the Saints goal 
Ibrahimovic na Pogba wakiangalia shuti la kichwa la mshambuliaji huyo wa PSG ukitinga wavuni
The 34-year-old Swede leaps with joy as his 36th-minute header gives United the lead as Old Trafford erupts 
Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 34 akishangilia bao la kwanza
The United forward is mobbed by team-mates after his stunning opening strike gave United an early advantage 
Ibrahimovic akipongezwa na wenzake 
United defender Luke Shaw takes a tumble in the Southampton box leading to penalty
Beki wa United  Luke Shaw akiangushwa na kuwa penalti
Ibrahimovic steps up to convert the resulting penalty as United take a 2-0 lead against the Saints
Ibrahimovic anafunga kwa penalti
Ibrahimovic celebrates in front of the United faithful as Jose Mourinho's side make it two from two in the opening weeks 
Ibrahimovic akishangilia mbele ya mashabiki wa United

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *