JOSE MOURINHO AJIPA MWEZI MMOJA KUICHUNGUZA MANCHESTER UNITED

KOCHA mwenye maneno mengi na tambo, Jose Mourinho amejipa mwezi mmoja kuichunguza Manchester United ili kujua kama anaweza kubaki na wachezaji hao ama awapige bei na kusajili wengine.

Mourinho aliyeipa Man United ubingwa wa Ngao ya Jamii wikiendi iliyopita, jana alikuwa ugenini kuiongoza timu hiyo katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England tangu atue Old Trafford.

United walikuwa wageni wa Bournemouth waliolala 3-1 na Mourinho ambaye amekiimarisha kikosi chake kwa kuwasajili Paul Pogba Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na mshambuliaji mkongwe, Zlatan Ibrahimovic, amesema uchunguzi wake hautachukua muda mrefu.

“Nitatumia mwezi mmoja tu kukichunguza kikosi hiki na kujua kama kinaweza kunipa mafanikio ama la,” alisema Mourinho.


Mourinho bado hawaamini baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na watangulizi wake; David Moyes na Louis Van Gaal ambao walitumia mamilioni ya pauni kuwanunua Marouane Fellaini, Radamel Falcao na Anthony Martial lakini biashara yao ikadoda.

No comments