JOSE MOURINHO ASEMA USHINDI NI KITU MUHIMU ZAIDI KWAKE

KOCHA Jose Mourinho anaamini kuwa kushinda mechi ni muhimu kwa Manchester United kuliko kuwa na mfumo maalum wa uchezaji.

Hata hivyo, Mourinho kma ilivyo kwa makocha wengine, angependa kufanikiwa akiwa na staili maalum ya uchezaji, lakini ameitazama United takriban robo muongo uliopita na anaona ushindi ndio kila kitu ukifuatiwa na mfumo.

“Nimekulia katika soka kama kocha tangu 2001 zaidi ama chini ya hapo na zaidi nilipokuja England mwaka 2004, niliona Manchester United kama timu ya ushindi, na si timu ya kushambulia,” alisema  jana kuelekea mechi yao ya leo dhidi ya Bournemouth waliyoibuka na ushindi wa mabao 3-1.

 “Nimeshacheza mara kadhaa dhidi ya Manchester United na ilikuwa timu ya kujilinda. Niliongoza Real Madrid dhidi ya Manchester United jijini Madrid na iliwapita safu ya viungo mara mbili… Wayne Rooney alicheza kushoto kumzuia beki wangu wa kulia.”

“Niliwaona mara zote kama timu ya ushindi kwa falsafa yao ya kushambulia, lakini ikawa ni timu ya ushindi. Timu ya ushindi inahitaji kufunga mabao mengi kuliko inayoruhusu kufungwa, lakini kama unataka kuruhusu mabao mengi kuliko unayofunga.”


“Hivyo changamoto ya Manchester United kujaribu kushinda katika zama mpya za Ligi Kuu England ni vigumu zaidi kuliko mkabla ya hapo. Hivyo ukweli kazi yangu ni ngumu sana lakini tunahitaji kushinda mechi, tunahitaji kushinda mashindano na kushinda ni nje ya namna ambavyo unaweza kucheza vibaya, lakini kushinda mashindano unahitaji kucheza vizuri.”

No comments