JUAN MATA AMWAMBIA MOURINHO "YALIYOTOKREA CHELSEA TUYAACHE KULEKULE"

“MIMI naishi kwa matumaini makubwa kwamba Mourinho ni kocha bora, kama akiona sifai kama ilivyokuwa wakati niko Chelsea, maana yake ni moja tu kuwa sitakiwi kukutana na kocha huyu mahali kokote katika timu yoyote,” amesema Mata.

Mchezaji huyo amedokeza kuwa anataka kucheza soka kwasababu ndio ajira yake na kwamba ikitokea kuwa hatakiwi kucheza kwa sababu yoyote ile, tafsiri yake ni kwamba anatakiwa ajitazame upya.

“Sina ugomvi na kocha Mourinho, najua hata yeye atakuwa anafahamu kuwa ni jambo jema kufanya nae kazi tena. Sijui kama atakuwa na sera zilezile. Nadhani yaliyotokea Chelsea tuyaache kulekule,” amesema.

Hayo ni maneno ya Juan Mata mara baada ya kuhojiwa na Sky Sports muda mchache mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ngao ya Jamii iliyowakutanisha Manchester United dhidi ya Leicester City.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa United kushinda mabao 2-1 na kutwaa Ngao ya Jamii, Mata aliingia dimbani akitokea benchi, lakini akajikuta akicheza kwa dakika chache tu na kutolewa tena na kocha Jose Mourinho.

Hatua hiyo iliwashangaza wengi na alipoulizwa ndipo akajibu: “Sina la kusema ingawa ninachoweza kusisitiza ni kwamba bado ninaishi kwa matumaini nikiwa hapa.”

Mata ambaye hakuwa katika wakati mzuri wakati wa kocha Mdachi Louis Van Gaal, amesema kwamba ujio wa Mreno huyo katika kikosi hicho umekuwa na matumaini ya nusdu kwa nusu ya kuendelea kuaminika katika kikosi cha kwanza.

Mata ni alama muhimu katika klabu ya Old Trafford, lakini katika namna nyingine, mchezaji huyo anaweza kuwa katika wakati mbaya zaidi.

Alikuwa katika kiwango bora kabisa katika Stanford Bridge na alifanya kazi yake kwa kiwango cha juu sana, lakini Mourinho alipochukua kazi, akampiga mkeka na nafasi yake ikawa inachezwa na Oscar kiasi kwamba Mata akauzwa katika kikosi cha Manchester United.

Lakini Mata majuzi amesema kwamba hana uhakika yale yaliyojitokeza katika kikosi cha Chelsea yatajirudia katika Manchester United.

No comments