KARAMA TONY MPIGA BASS WA SIKINDE ANUSURIKA KUFA KWA AJALI YA GARI


MPIGA bass wa kutegemewa wa Mlimani Park Orchestra "Sikinde Ngoma ya Ukae", Karama Tony amenusurika kufa baada ya gari alilikuwa akiendesha kupinduka na kubiringita mara mbili.

Karama ameithibitishia Saluti5 kuwa ni kweli amepata ajali leo saa 10 alasiri lakini anamshukuru Mungu yuko salama salmin.

“Nilikuwa natokea huko uzaramnuni Kisarawe nilipofika maeneo ya Masaki gari langu lilipinduka na kubiringita mara kadhaa lakini kwa bahati nzuri nilikuwa nimefunga mkanda na hiyo ndiyo ikawa salama yangu.


“Nimefanikiwa kuliondosha gari eneo la tukio na nimelipaki Chanika, nikifika mjini ntaenda kufanya vipimo ili kujua kama ni majereha kwa ndani,” alisema Karama aliyekuwa akiendesha gari aina ya Suzuki Carry maarufu kama Kirikuu.

No comments