KLOPP: NAHITAJI MLINDA MLANGO WA KIWANGO CHA KUISAIDIA TIMU

BOSI mpya wa Liverpool, Jurgen Klopp amekiangalia kikosi chake cha sasa kasha amekuja na kauli moja kwamba bado anahitaji kuwa na mlinda mlango wa kiwango cha kuisaidia timu.

Kauli ya Klopp inakuja siku chache baada ya kucheza mechi nyingi za majaribio kujiandaa na premier ya msimu unaoanza Agosti 20 nchini England.

“Ninahitaji kuendelea kusuka kikosi japo dirisha la usajili limefungwa, ila ninahitaji kutupia macho katika suala la kipa. 
Lakini sio mlinda mlango tu bali lazima niwe na muda wa kuangalia vigezo na viwango ili mwisho wa siku nipate mlinda mlango aliye bora,” alisisitiza Klopp.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuiongoza timu yake katika mechi za majaribio kabla ya kuanza kwa Ligi ya premier.

“Nimekamilisha usajili wa msimu huu, lakini macho yangu hayatalala. Nitaweka katika orodha yangu wachezaji wengi kwa ajili ya usajili ujao.”

“Nafikiri tunahitaji mlinda mlango kwa kiasi kikubwa, inategemea na aina ya mahitaji kwa sasa,” alisema Klopp.

“Sisi ni kati ya klabu kubwa hivyo hata aina ya wachezaji lazima wawe bora kulingana na ukubwa wa timu tulizonazo.”

“Ninaweza nikaficha ukweli huu sasa, lakini baadae ninaweza nikajisuta mwenyewe kama nitaendelea kujiaminisha kuwa nina kikosi bora. Hapana, tunahitaji wengi walio bora akiwemo mlinda mlango,” amesisitiza Klopp ambaye ni kocha wa zamani wa Borussia Dortmund ya Ujerumani.

No comments