Habari

KOCHA BENITEZ AMUONYA MOUSSA SISSOKO ASITHUBUTU KWENDA REAL MADRID

on

BOSI wa Newcastle United,
Rafael Benitez amemuonya straika Moussa Sissouko kuacha mpango wa kutaka kutua
Real Madrid.
Sababu ya onyo hilo ni kile
alichodai kocha huyo kuhofia kwenda kuua kiwango chake kwani ushindani wa namba
ndani ya Madrid ni mkubwa.
Sissoko amekuwa katika rada za
Real Madrid tangu kumalizika kwa michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini
Ufaransa.
Katika michuano hiyo, Sissoko
alionyesha kiwango cha hali ya juu hivyo kuzivutia timu mbalimbali ikiwemo
Madrid.
Sissoko mwenye umri wa miaka
26, amekuwa akiwindwa na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa dau
la euro mil 40.
“Natambua Real wanataka kuja
kwangu. Ninawasubiri, najua wanakuhitaji sana kwa sasa.”
“Lakini ninachoweza kuona ni
kwamba ndani ya Madridi kuna ushindani mkubwa wa namba.”
“Unaweza ukafurahia kwenda kule
leo, lakini kesho ukaenda kujutia uamuzi wako, lakini itakuwa tayari
umeshachelewa,” alisisitiza Benitez.
Hata hivyo, Benitez
alithibitisha kuwa klabu yake ya Newcastle haitakubali kumuuza straika huyo
chini ya dau la euro mil 40, kwani bado ana mkataba wa miaka miwili kamili.
“Nimemwambia Moussa, tunafahamu
mambo yanavyokwenda ndani ya soka la kisasa na hatua ya kukurupuka sio njia
njema, bali ni kutafakari,” amenukuliwa bosi huyo wa zamani wa Los Blancos.

Madrid wameingia katika mbio za
kutaka kumnasa Sissoko kufuatia hatua yao ya kumkosa Pogba ambaye tayari ametua
katika kikosi cha mashetani wekundu wa jiji la Manchester.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *