KUMBE WACHEZAJI LEICESTER CITY WALITENGENEZA KUNDI LA WHATSAPP KUMSHAWISHI N'GOLO KANTE ABAKI

WACHEZAJI wa Leicester City wamefichua kwamba walianzisha kundi la WhatsApp kwa lengo la kumshawishi kiungo N’Golo Kante asiihame klabu hiyo lakini mpango huo ulishindikana.

Kante ndiye mchezaji mkubwa aliyesajiliwa na Chelsea kwa kitita cha pauni mil 32 kutoka kwa mabingwa hao ambao walishangaza dunia kwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita.

Wachezaji wa Leicester City, Danny Simpson, Marc Albrighton na Christian Fuchs walieleza kwa kirefu jinsi walivyokuwa wakishawishi wenzao wasiihame timu hiyo ili wawe wote msimu ujao.

“Kulikuwa na kundi la WhatsApp lakini kama mchezaji anataka kuondoka basi huwezi kumzuia,” alisema Albrighton.

“Tulimtumia Kante meseji nyingi, kila mmoja akimtakia kheri… kabla ya kumuondoa kwenye kundi hilo,” aliongezea Simpson.


“Tulishawishi lakini tulishindwa,” Fuchs alisema.

No comments