LICHA YA KUSHINDA 5-0, JURGEN KLOPP BADO ANAKIOTA KIPIGO CHA BURNLEY


Jurgen Klopp has said he would prefer to play Daniel Sturridge in a central striking role

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp amesema bado anaendelea kufadhaishwa na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu wikiendi iliyopita, lakini akadai bado ana matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu. 

Klopp amesema licha ya Jumanne usiku kushinda 5-0 dhidi ya Burton Albion kwenye Capital One Cup, lakini bado kuachia pointi tatu kwa Burnley kumempasua kichwa.

Liverpool walianza msimu huu vizuri kwa kupata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Arsenal lakini wakashindwa kutamba kwa Burnley kufuatia magoli ya Sam Vokes na Andre Gray.


No comments