LUKAS PODOLSKI ATUNDIKA DARUGA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

STRAIKA wa timu ya taifa ya Ujerumani, Lukas Podolski amethibitisha kuachana na timu hiyo kuanzia sasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Podolski ambaye kwa ngazi ya klabu, anaichezea timu ya Galatasaray, kutangaza mwaka jana kuwa fainali za mataifa ya Ulaya “Euro 2016” ndizo zitakazokuwa mashindano yake makubwa ya mwisho akiwa na timu ya taifa.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, alikuwemo kwenye kikosi cha kocha Joachim Low na aliweza kucheza mchezo mmoja ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Slovakia katika hatua ya makundi.

Ujerumani waliondolewa kwenye mashindano hayo kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ufaransa katika hatua ya nusu fainali na Podolski ndipo alipomueleza kocha wake kuhusu uamuzi huo.


“Kabla ya msimu wa mechi kuanza tena ningependa kuwasiliana nanyi mashabiki. Ninataka kumweleza kocha kuwa kuanzia asa sitaweza kuchezea tena timu ya taifa,” alisema mchezaji huyo kupitia mtandao wake wa kijamii.

No comments