MACHO YOTE LEO USIKU KWA LILIAN INTERNET NA TWANGA PEPETA MANGO GARDEN …Asha Baraka kuwa MC


LEO ndio ile siku ya kwenda kuona vile viono vya akiba vya Lililan Internet katika onyesho maalum litakalofanyika Mango Garden Kinondoni.

Mnenguaji huyo maarufu wa Twanga Pepeta, leo ataachana rasmi na kazi ya unenguaji akihitimisha miaka yake 17 ya kazi hiyo.

Kwa kuthamini mchango na uwezo wake, Twanga Pepeta wameamua kuandaa onyesho hilo maalum la Lilian Internet kuagana na unenguaji.

Ikumbukwe kuwa Twanga Pepeta ndiyo inayobeba sehemu kubwa ya maisha ya kisanii ya mnenguaji huyo.

Mwenyewe Lilian aliiambia Saluti5 kuwa siku hiyo ataaga mashabiki wake kwa kutumia viuno vyake vya akiba ambavyo hajawahi kuvionyesha jukwaani hata mara moja.

“Nitawaaga mashabiki wangu kwa vitu vya adimu, nina mauno na staili za unenguaji ambazo sikuwahi kuzionyesha hapo kabla, ilikuwa ni akiba yangu kwa siku maalum kama hii, Hivi ndivyo alivyosema alisema Lilian Internet wiki iliyopita.

Tayari mashabiki wa dansi wameshapandwa na mzuka wa kwenda kuona viuno hivyo vya akiba.

Kama vile hiyo haitoshi, mkurugenzi wa Twanga Pepeta mamaa Asha Baraka ndiye atakayekuwa MC wa onyesho hilo hususan katika kipengele kitakachompandisha Lilian Internet jukwaani.

No comments