MAN FONGO AKATAA KUITWA MFALME WA SINGELI


STAA wa nyimbo “Hauna” na “Hainaga Ushemeji” Man Fongo amekataa kuitwa mfalme wa muziki wa singeli.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anaipeperusha vilivyo bendera ya muziki huo wa kiswazi, amesema hapendi kujitukuza na kukubali kupewa majina makubwa na badala yake angependa kujulikana tu kama mwakilishi wa singeli.

Akizungumza na kipindi cha “Plate Number” cha Azam Two, Man Fongo alisema: “Mimi bado mchanga na sijafikia hatua kubwa ya kujulikana nje ya mipaka ya Tanzania na hivyo sipendi kujikweza na kupokea majina makubwa kama ya mfalme na mengine mengi.

“Cha msingi ninachotaka ni kuendelea kuupigania muziki huu ambao wananchi wameanza kuuelewa ili uvuke mipaka ya nchi”.

No comments