Aguero scored from the penalty spot after Raheem Sterling had been fouled in the box by Patrick van Aanholt
BEKI mpya wa Sunderland Paddy McNair aliyesajiliwa kutoka Manchester United, amejifunga dakika ya 87 na kuizawadia Manchester City bao la ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ulioshia kwa Sunderland kulala 2-1.

City ilitangulia kwa bao la mapema lililofungwa kwa penalti na  Sergio Aguero kunako dakika ya nne baada ya  Raheem Sterling kufanyiwa faulo na  Patrick van Aanholt.

Lakini Defoe akaisawazishia Sunderland dakika ya 71  na wakati watu wengi wakiamini matokeo yatakuwa sare, McNair akajifunga.

Matokeo ya mechi zote za Premier League zilizochezwa Jumamosi ni kama ifuatavyo:

Hull City 2 - 1 Leicester City
Burnley 0 - 1 Swansea City
Crystal Palace 0 - 1 West Bromwich Albion
Everton 1 - 1 Tottenham Hotspur
Middlesbrough 1 - 1 Stoke City
Southampton 1 - 1 Watford
Manchester City 2 - 1 Sunderland
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac