Habari

MANCHESTER UNITED BADO HAIJAMALIZA USAJILI …SASA YAPIGA SPIDI KUMNASA GABRIEL BARBOSA WA SANTOS YA BRAZIL

on

Gabriel Barbosa is interesting a number of clubs including Leicester City and Inter Milan
MANCHESTER UNITED ipo tayari kuwapiga bao wapinzani wake kwa kumsajili mshambuliaji Gabriel Barbosa wa Santos ya Brazil kwa pauni milioni 30.
Kocha Claudio Ranieri wa Leicester alikuwa akiamini kuwa ameshashinda vita ya kumsajili kinda huyo wa miaka 19 ambaye kwa sasa anatesa na Brazil kwenye michuano ya Olimpiki.
Lakini sasa Jose Mourinho anatajwa kuwa yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumpeleka  Old Trafford Gabriel Barbosa ambaye pia anawaniwa na Bayern Munich, Juventus, Inter Milan, Chelsea na Atletico Madrid.
Gazeti la The Sun la Uingereza linaandika kuwa United iko hatua moja mbele katika kukamilisha usajili huo ndani ya saa 48 zijazo. 
Manchester United wanahitaji mshambuliaji mwingine wa kumsaidia Zlatan Ibrahimovic  ambapo Mourinho anaamini kuwa Barbosa ni chaguo sahihi katika mapinduzi anayoyafanya Old Trafford.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *