Habari

MEMPHIS DEPAY ANA KIBARUA KIZITO KWA JOSE MOURINHO

on

Memphis Depay, pictured during Wayne Rooney's testimonial, must improve this season
Miezi 12 iliyopita, jina la Memphis Depay lilikuwa midomoni mwa kila mtu kufuatia uhamisho wake wa pauni milioni 25 kutoka PSV Eindhoven. Lakini sasa anapigania nafasi ya kuwa kwenye mipango ya Jose Mourinho na lolote linaweza kutokea kwake.
Depay alitarajiwa kuziba kabisa pengo lililoachwa na Ryan Giggs kwenye wingi ya kushoto ya Manchester United lakini ameshindwa kabisa kung’ara.  
Kwa sasa Depay anahitaji kuthibitisha ubora wake kabla Mourinho hajapiga panga lake na kumnyofoa yeyote katika kikosi chake cha wachezaji 26 aliowaamini.
Wengi waliingia hofu kuwa pengine ujio wa Henrikh Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund ungehitimisha huduma ya Depay ndani ya Manchester United, lakini bado Mourinho ameamua kumwamini na kumjumuisha kwenye kikosi chake cheye makipa watatu na wachezaji 23 wa ndani.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ana kazi nzito ya kupigania nafasi yake kwa Mourinho ambaye ameweka wazi kuwa katika mwanzo wa ligi hatapenda kutumia mfumo kubalisha badilisha kikosi chake cha kwanza.
Depay was given the legendary No 7 shirt by Louis van Gaal but he hasn't lived up to the hype
Depay alipewa jezi namba 7 yenye heshima kubwa Manchester United 
United supporters and Van Gaal were delighted with their new signing this time last year
Depay aliposajiliwa United  na Van Gaal msimu uliopita
Jose Mourinho has included Depay in his chosen 26-man squad despite last season's form
Jose Mourinho bado anamwamini Depay

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *