MO FARAH ANG'ARA OLIMPIKI RIO... awabwaga Wakenya na Waethopia mbio za meta 10,000

MKIMBIZA upepo mahiri, Mo Farah amekuwa mwanariadha wa kwanza wa Uingereza wa mbio za uwanjani kushinda nishani tatu za dhahabu katika michezo ya Olimpiki, baada ya kuwabwaga Wakenya na Waethopia katika mbio za meta 10,000 zilizofanyika jana mjini Rio.

Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 33, alijikwaa wakati wa mbio hizo japo alijikakamua vilivyo katika mita 100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27.5. mkenya Paul Tanui ameshinda nishani ya fedha, huku mwanariadha wa Ethopia, Tamirat Tola akimaliza wa tatu.

Farah atarejea uwanjani Jumatano kutetea taji lake la mbio za mita 5,000 aliloshinda miaka minne iliyopita mjini London.

“Nimeshinda dhahabu tatu kwa wanangu watatu,” Farah alisema. “Ningetaka kushinda dhahabu ya nne katika mbio za mita 5,000 kwa mtoto wangu mchanga.”

Iwapo atashinda mbio hiyo, atafikia mafanikio sawa nay a mwanariadha wa Finland, Lasse Viren aliyehifadhi mataji mawili ya Olimpiki katika mbio za mwendo mrefu mwaka 1976.


Hata hivyo, Mo Farah alipata ushindani mkubwa kutoka kwa Mkenya Paul Tanui na ilimbidi atumie nguvu za ziada kuongoza mbio hizo.

No comments