MOURINHO AMTAKA MEMPHIS DEPAY KUKAZA... asema amekusudia kumfanya awe sehemu ya kikosi chake

KOCHA mpya wa Manchester United, Jose Mourinho amemtaka nyota wake Memphis Depay kuhakikisha anafanya makubwa katika timu hiyo ikiwa ni baada ya kumchagua kuwa miongoni mwa wachezaji wake 23 aliowatangaza juzi kwa ajili ya mechi ya jana dhidi ya Bournemouth.

Awali watu wengi walikuwa wakitarajia kuwa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22 atakuwa miongoni mwa watakaopigwa panga na Mourinho bada ya kuonyesha kiwango kibovu katika msimu wake wa kwanza tangu alipotua Old Trafford, lakini kwa sasa kocha huyo anatarajia kupata makubwa kutoka kwa staa huyo.

“Kwa ujumla nataka Memphis kuwa sehemu ya kikosi chake,” Mourinho aliliambia gazeti la Sunday People.

“Sitaki kuzungumzia yaliyojitokeza msimu uliopita, lakini namfahamu ni mchezaji ambaye niliwahi kumuona akiwa na PSV na katika fainali za Kombe la Dunia miaka miwili iliyopita,” aliongeza kocha huyo.


Alisema kwamba, anapokuwa ameshamwingiza akilini mwake mchezaji mara zote huwa anapenda kukaa nae kutokana na kwamba anamuona ni kijana mwenye tabia nzuri na akasema kuwa hajali kile ambacho watu wanakisema.

No comments