MOURINHO AWAPONDA WAPINZANI WAKE KWA KUOGOPA KUWA WAZI KUHUSU KUCHUKUA UBINGWA

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amewaponda wapinzani wake kwa kuogopa kuwa wazi kuhusu nia zao za kuchukua ubingwa, akidai kuwa timu yake haina woga linapokuja suala la kuweka wazi nia hiyo.

United ilimpa kibarua Mourinho baada ya kumtimua Louis Van Gaal, siku sita tu baada ya kunyakua taji la FA mwezi Mei na viongozi wa labu hiyo wamekuwa mstari wa mbele kumsaidia kocha huyo katika suala zima la kusajili ambao wamemnasa kiungo Paul Pogba kutoka Juventus, Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.

“Sisi Man United tumeshaweka wazi nia yetu tangu siku ya kwanza kuwa tunataka ubingwa, wapinzani nao nadhani wanawaza kama sisi, lakini wanaogopa kusema wazi.”
“Hilo kwetu halipo,” alisema.


United imeanza msimu huu na ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuwachapa mabingwa wa Ligi Kuu England, Leicester City mabao 2-1 wikiendi iliyopita ambapo Jumapili wamepata ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi dhidi ya Bournemouth.

No comments