MSONDO, KHADIJA KOPA KUSINDIKIZA UZINDUZI WA DAR MUSICA SEPTEMBA 16 MANGO GARDEN


BENDI ya Dar Musica inatafanya uzinduzi wake rasmi Ijumaa ya Septemba 16, kwenye ukumbi wa Mango Gardeni, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo utakaoenda sambamba na utambulisho wa albam “Chozi la Masikini”,  utasindikizwa na  malkia wa mipasho Khadija Kopa pamoja na bendi ya Msondo Ngoma.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana mchana, meneja wa bendi hiyo Hamis Maero alisema kuwa uzinduzi huo mkubwa unafanyika kwa mara ya kwanza toka rais mpya Jado FFU aingie madarakani.

Hamis alisema kuwa utambulisho huo pia utatumika kwa ajili ya kutambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hiyo.

Naye rais wa bendi hiyo Edward Anthony “Jado FFU” alisema kuwa nyimbo zitakazotmbulishwa katika uzinduzi huo ni pamoja na wimbo uliobeba albamu yao ya “Chozi la Maskini” pamoja na “Salmaga”.

Nyimbo nyingine ni “Bongo mchongo”, “Maisha Upendo”, “Mtu Box”, “Jibebishe”  na “Ama zao Ama zangu”.
Dar Musica kuzinduliwa rasmi Septemba 16
 Kiongozi wa Bendi ya Dar Musica,  Edward Anthony "Jado FFU" (kushoto) akizungumzia uzinduzi rasmi wa bendi yao, unaotarajia kufanyika Septemba 16, kwenye ukumbi wa Mango Garden ulipo Kinondoni Dar es Salaam.
Jado akisisitiza jambo fulani. Kulia ni meneja wa bendi Hamis Maero

No comments