MUETHOPIA ALMAZ AYANA AWA WA KWANZA KUIPA AFRIKA DHAHABU RIO DE JANEIRO

MWANARIADHA wa kike wa Ethopia, Almaz Ayana amekuwa mwanamichezo wa kwanza kulipa bara la Afrika Medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo inayoendelea ya Olimpiki mjini Rio.

Mbali ya kutwaa medali ya dhahabu, pia mwanariadha huyo alifanikiwa kuvunja rekodi ya Dunia katika mbio za mita 10,000 kwa upande wa wanawake.

Ayana mwenye umri wa miaka 24, aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na kuendelea kuwatimulia vumbi hadi mwisho, saa kubwa ikionyesha ametimka kwa dakika 29:17.45 ikiwa ni rekodi mpya ya Dunia.


Awali rekodi iliyowekwa kwa mbio hizo ilikuwa ya dakika 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Juuxia mwaka 1993, aidha Mkenya Vivian Cheruiyot alishika nafasi ya pili na kutwaa medali ya fedha huku staa mwingine wa Ethopia, Tirunesh Dibaba akishika nafasi ya tatu na kutuzwa medali ya shaba.

No comments