MWANARIADHA CASTER SEMENYA ASEMA ANAJITOA MBIO ZA MITA 400

MWANARIADHA wa kike wa Afrika Kusini anayetesa katika mita 400, 800 na 1500, Caster Semenya amesema kuwa anajitoa katika mbio za mita 400 ili kuweka nguvu kwenye mita 800.

Semenya ambaye alifuzu mbio hizo tatu tofauti, amesema katika michuano ya Rio amepanga kuelekeza nguvu kwenye mita 800.

Hata hivyo, hakutoa sababu za kujitoa katika mita 400 ambako alitarajiwa kutwaa medali ya dhahabu sawa na katika mita 800.


Bingwa huyo wa Dunia wa mita 400 na 800, alipata kuzushiwa kashfa ya jinsi kutokana na kasi yake kuwatesa washiriki kutoka barani Ulaya.

No comments