MWANARIADHA KARIMAN ABULJADAYEL WA SAUDI ARABIA AANDIKA HISTORIA RIO

MKIMBIAJI wa mbio fupi Kariman Abuljadayel amekuwa mwanamke wa kwanza kutoka Saudi Arabia kushiriki katika mbio za meta 100 katika michuano ya Olimpiki.

Abuljadayel, 22, aliyekuwa amevalia vazi la kujifunika mwili pamoja na hijabu, hakufanikiwa kufuzu baada ya kumaliza akiwa nafasi ya saba kundi la tatu la wanariadha wanane walioshindana hatua ya awali ya kufuzu, akitumia muda wa sekunde 14.61.

Raia wa Afghanistan, Kamia Yousufi pia alikimbiza akiwa amevalia hijabu na vazi la kufunika vyema mwili na ndie aliyemaliza wa mwisho kundi hilo muda wake ukiwa sekunde 14.02.

Mwanariadha wa mbio za wastani, Sarah Attar alikuwa mwanamke wa kwanza kuwakilisha Saudi Arabia kwenye mashindano ya mbio Olimpiki aliposhiriki michezo ya London 2012.


Saudi Arabia ilikuwa imewapiga marufuku wanawake kushiriki Olimpiki lakini marufuku hiyo ikaondolewa mwaka 2012.

No comments