MWANARIADHA SILVIA DANEKOVA ATIMULIWA RIO KWA KUFELI VIPIMO VYA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI

MWANARIADHA wa kuruka viunzi anayeshikilia ubingwa wa dunia wa mita 3,000, Silvia Danekova wa Denmark amefeli vipimo vya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Mchezaji huyo mwenye miaka 33, ametimuliwa katika michuano ya Olimpiki baada ya vipimo kuonyesha kuwa alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu.

Mamlaka zimesema mchezaji huyo alifanyiwa vipimo vya afya siku tatu tu baada ya kutua Brazil, Julai 26, mwaka huu kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo.

Kutokana na kile alichodhani kama ni kudhalilishwa, mchezaji huyo hakutaka kukata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya kimichezo (CAS), badala yake amerejea nyumbani.

Kutokana na hilo, shirikisho la riadha la kimataifa (LAAF), linasubiriwa kwa ajili ya kuamua adhabu ya kumpa mwanariadha huyo.

No comments