MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Ahmed Olotu “Mzee Chilo” amesema sio kweli kwamba wasambazaji wa Kihindi wanawanyonya wasanii wa filamu.

Akizungumza na Saluti5, Mzee Chilo amesema kuwa wasanii wengi kwa sasa wanafanya filamu mbovu ndio maana wanakosa soko kwa Wahindi.

“Wanaosema kwamba Bongomuvi imeshuka sijui hizi taarifa wanazipata wapi, mimi nipo kwa miaka mingi na wasambazaji wa Kihindi na sijawahi kupata tatizo lolote kusema kweli,” alisema Chilo.

“Mimi nadhani  wanaosema Wahindi wanaharibu soko la filamu siyo kweli, huo ni uongo, wao ndio wanafanya filamu mbovu ndio maana hazifanyi vizuri.”


Mwigizaji huyo amewataka wasanii wa filamu kufanya kazi kwa bidii na kuacha kulalamika.
NENDA PLAY STORE KUPITIA SMART PHONE YAKO KISHA DOWNLOAD APP YETU YA "SALUTI5">>>> BONYEZA HAPA
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac