Habari

PICHA 10: MZEE YUSSUF APAA KWENDA HIJJA …asisitiza bye bye muziki

on

Aliyekuwa mfalme wa taarab Mzee Yussuf amepaa kwenda Makka kuhiji.
Mzee Yussuf ambaye kwa sasa anapenda ajulikane kama ‘Ustadh’ badala ya
‘Mfalme’ amepaa na ndege ya Emirates mchana huu.
Ustadh Mzee Yussuf ambaye hivi karibuni alitangaza kuachana na muziki
wa kidunia, amesisitiza kuwa uamuzi wake huo hautabadilika kamwe.
Saluti5 iliyokuwepo uwanja wa ndege – Julius Nyerere International Airport, jijini Dar es Salaam, ilishuhudia watu wengi waliokuwa wakisindikiza ndugu zao wakihamasika
na kumpongeza Mzee Yussuf kwa uamuzi wake wa kwenda Hijja.
Pata picha 10 za Mzee Yussuf akiagana na ndugu na jamaa Julius Nyerere International Airport.
 Mzee Yussuf akiwa na mkewe Leyla Rashid
 Waimbaji wa Jahazi Fatma Mcharuko (kushoto) na Leyla Rashid wakiwa Airport kumsindikiza Mzee Yussuf
 Baba mzazi wa Mzee Yussuf naye alikuwepo kumuaga mwanaye
 Mzee Yussuf katika picha ya pamoja na ndugu na jamaa
 Mzee Yussuf akiagana na mkewe Leyla Rashid
 Mkurugenzi wa East Africa Melody Ashraf Mohamed akimwaga Mzee Yussuf
 Mtu na wajina wake …Mzee Yussuf na Yussuf Mdoe wakiagana
 Said Mdoe, Mzee Yussuf na Leyla Rashid
Mzee Yussuf akijiandaa kuingia chumba cha wasafiri

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *