Habari

PICHA 14: WASANII WA MUZIKI NA FILAMU WAJITOKEZA KUPINGA OPERESHENI “UKUTA”

on

WASANII wa fani mbali mbali wamejitokeza kupinga Operesheni UKUTA
iliyopangwa kufanywa na Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) Septemba Mosi mwaka huu.
Wakiwakilisha fani za muziki na filamu, wasanii hao wakafanya mkutano
na waandishi wa habari ndani ya mgahawa ulioko kwenye jengo la Dar Free Market
jijini Dar es Salaam na kuitaka CHADEMA isitishe mpango kwa kuwa utaleta
uvunjivu wa amani.
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka akawataka Chadema na vyama vya
siasa kwa ujumla watafute suluhu kwa kujikita kwenye meza za mazungumzo badala
kulazimisha kufanya maandamano yasiyo na kibali.
Chadema imetangaza nia yake ya kufanya maandamano nchi nzima Septemba
Mosi katika kile wanachokiita ni Umoja wa Kuzuia Udikteta Tanzania (UKUTA),
mpango ambao umepingwa vikali na Jeshi la Polisi.

Steve Nyerere aliyekuwa akiiwakilisha tasnia ya filamu, amesema
mpango huo haufai na watakaoandamana watawasumbua bure ndugu zao kuwapelekea
chakula magerezani na mahospitalini.
“Uchaguzi umekwisha na tumeshampata rais wetu ambaye pia ndiye Amiri Jeshi mkuu, ni vyema wanasiasa wakaheshimu mamlaka zilizoko na kutumia njia za kidiplomasia kuwasilisha madai yao,” alisema Steve Nyerere.
Kauli mbiu ya wasanii hao ilikuwa ni “Nchi Yetu, Amani Yetu”.
 Mstari wa mbele kutoka kushoto ni Khadija Kopa, Asha Baraka, Steve Nyerere na Siza Mazongela
 Mkutano ukiendelea
 Wasanii mbali mbali katika mkutano na waandishi wa habari
 Asha Baraka akisisitiza jambo
 Ukuta yapingwa na wasanii
 Steve Nyerere akifafanua jambo
 Wasanii wametaka wapinzani watumie njia za kidiplomasia kuwasilisha madai yao
 Khadija Kopa (Kushoto) naye akiongea kuhusu kupinga Ukuta
 Ally Chocky akitoa hoja
Wasanii na wadau wa sanaa wakisikiliza hoja kwa makini

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *