PICHA 15: MALKIA LEYLA RASHID ALIVYOLISONGESHA JAHAZI JANA USIKU NDANI YA MANGO GARDEN


TOFAUTI na ilivyoripotiwa na gazeti moja katikati ya wiki kuwa Leyla Rashid naye amestaafu muziki kama mumewe Mzee Yussuf, lakini mwimbaji huyo alitesa vilivyo jana usiku ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.

Malkia Leyla aliungana na waimbaji wenzake nyota kama Khadija Yussuf, Prince Amigo, Miriam Amour na Fatma Mcharuko katika onyesho hilo la Jahazi lililoshuhudia bonge la ‘playlist’ la nyimbo bora kabisa za taarab.

Waimbaji wengine mastaa wa Jahazi waliokuwepo Mango Garden ni Rahma Machupa, Aisha Vuvuzela, Mishi Mohamed, Fatma Kassim, Mwasiti Mbwana na Mohamed Ally “Mtoto Pori”.

Hivi karibuni Mzee Yussuf alitangaza kumrudia Mwenyezi Mungu na kuachana na muziki wa taarab ambapo swali kubwa likawa ni je mkewe (Leyla) naye ataachana na muziki ili kumuunga mkono mumewe?

Gazeti moja kubwa la michezo na burudani likamnukuu Leyla katikati ya wiki akisema na yeye ameamua kuachana na muziki, lakini katika kuonyesha kuwa hatua hiyo bado haijafikiwa, malkia Leyla Rashid alikuwepo Mango Garden na kukamua nyimbo mbili “Fanya Yako” na “Nina Moyo sio Jiwe”.

Hata hivyo, Leyla alikuwa wa mwisho kuingia ukumbini na wa kwanza kuondoka - aliingia saa 6 usiku na kuondoka saa 8 wakati onyesho likiendelea hadi saa 9 usiku.

Pata picha 15 za onyesho hilo la Jahazi ndani ya Mango Garden.
 Fatma Kassim
 Chiriku Hadija Yussuf
 Malkia Leyla Rashid
 Leyla akiwachezesha mashabiki wake
 Rahma Machupa
 Layla Rashid alivyotokelezea 
 Mohamed Mauji katik solo
 Fatma Mcharuko
 Mgeni Kisoda akipagawisha na gitaa la bass
 Fatma Mcharuko alivyotoka bomba na kivazi chake
 Mohamed Ali "Mtoto Pori" akitesa na wimbo "Tupendane Wabaya Waulizane" wa Mzee Yussuf
 Mwimbaji wa Mashauzi Classic Abdulmalick Shaaban akishuhudia onyeshola Jahazi
 Aisha Vuvuzela "Mtoto wa Uswahilini" akilimiliki jukwaa
 Baadhi ya waimbaji wa Jahazi
Jamila Dolphin (kushoto) akiwa na Mwanne Othman mtangazani wa East Africa Radio

No comments