Habari

PICHA 20: JAHAZI ILIVYOMEREMETA BILA MZEE YUSSUF KATIKA UZINDUZI WA VIDEO MPYA …nyomi si la kitoto Travertine Hotel

on

JUMAPILI usiku ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni jijini
Dar es Salaam, Jahazi Modern Taarab walifanikiwa kuzindua video mpya kwa
kishindo kikubwa.
Umati mkubwa wa mashabiki ukafurika ukumbini humo kushuhudia uzinduzi
huo wa video ya albam ya “Kaning’ang’ania”.
Hili linakuwa ni onyesho lililofana zaidi tangu mkurugenzi wao Mzee
Yussuf alipotangaza rasmi kustaafu muziki wiki kadhaa zilizopita.
HABARI WANAYO! Hiyo ikawa ndio kauli mbiu ya Jahazi katika onyesho
hilo ikiwa ni salam kwa wale wanaodhani kundi hilo litayumba bila Mzee Yussuf.
Wenyewe wakaenda mbali zaidi kwa kusema: “Hii ndiyo Barcelona, kaondoka Messi lakini moto uko pale pale”.
Hata hivyo kwa wale mashabiki waliotaka kununua DVD za video hiyo ya
Kaning’ang’ania ukumbini hapo, walilazimika kurudi mikono mitupu kwa kuwa DVD
hizo hazikuwepo kutokana na kuchelewa kuwekwa stamp za TRA na badala yake
zitaanza kuuzwa katikati ya wiki hii.
Kulikuwa na wakati ulioteka hisia za watu – ni pale kipande cha video
ya wimbo “Kaning’ang’ania” wa Mzee Yussuf kilipoachiwa kwenye screen kubwa – Watu
walishangilia sana.
Kabla ya wimbo huo mashabiki walionyesha kiu yao kwa Jahazi kwa kukataa kabisa kusimamishwa kwa show kwaajili ya kupisha uonyeshwaji wa video ya nyimbo hizo na badala yake walitaka
burudani iendelee na ikabidi nyimbo hizo kupigwa ‘live’ huku screen  zikionyesha
video isiyo na iliyozimwa sauti (mute).
Lakini ilipofika zamu ya wimbo wenyewe wa “Kaning’ang’ania” mashabiki
walikubali kurejesha macho yao kwenye screen kubwa kuitazama video hiyo huku
burudani ya jukwaani ikiwa imesimama kwa dakika chache.
Pata picha 20 za onyesho hilo la uzinduzi wa video mpya ya Jahazi
Modern Taarab.
 Mohamed Mauji
 Prince Amigo akipagawisha mashabiki
 Babu Ali “Kichupa” kwenye kinanda
 Rahma Machupa
 Mkurugenzi wa Jahazi Hamis Boha (kushoto) akionyesha audio CD ya albam ya “Kaning’ang’ania”
 Malkia Leyla Rashid akifanya yake jukwaani
 Mishi Mohamed jukwaani
 Mishi akipagawisha mashabiki
 Leyla akiimba mbele ya umati mkubwa wa watu
 Tofauti na wengi wanavyovumisha kuwa Leyla ameacha muziki, lakini mwimbaji huyo bado anaendelea kutesa na Jahazi
 Fatma Mcharuko
 Msanii wa Bongo Movie Kupa akisalima mashabiki
 Mwana mpotevu Mwasiti Robert MC maarufu wa Jahazi naye alikuwepo kazini baada ya kupotea kwa muda mrefu kutokana na safari zake za nje ya nchi
 Huu ndiyo umati uliofurika Travertine Hotel
 Aisha Vuvuzela
 Vuvuzela akiimba moja ya nyimbo za Jahazi
 Waimbaji wa Jahazi jukwaani
Safu nzima ya waimbaji wa kike wa Jahazi Modern Taarab

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *