Habari

PICHA 35: RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BI SHAKILA SAID …Mama Samia Saluhu aongoza waombolezaji

on

HATIMAYE mwili wa mwimbaji mkongwe wa taarab Tatu Said maarufu kama
Shakila Said umehifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo saa 10 alasiri.
Mazishi ya Bi Shakila aliyefariki jana usiku, yamefanyika katika
makaburi ya Charambe, jijini Dar es Salaam mwendo mfupi kutoka nyumbani kwake.
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu aliongoza mamia ya waombolezaji
waliofika nyumbani kwa marehemu Shakila ambaye alifariki ghafla baada ya
kudondoka muda mfupi baada ya kupata sala ya magharibi.
Aidha, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye naye alikuwepo msibani na akaongoza waombolezaji wa kiume kuelekea
makaburiki kumzika Bi Shakila kwa taraibu zote za dini ya Kiislam.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Dr. Jakaya Kikwete yeye
alipitiliza moja kwa moja makaburini kushiriki mazishi kabla ya kwenda nyumbani
kwa Bi Shakila kujumuika na wafiwa na kuwapa pole.
Kikwete alibadilisha hali ya hewa nyumbani kwa marehemu kwa hamasa ya
aina yake na ya kusisimua baada ya waombolezaji kumshangilia kwa nguvu mara tu
aliposhuka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwa mguu.

Kwa sekunde kadhaa ni kama vile waombolezaji waliusahau msiba kwa
faraja ya kumuona rais mstaafu.
Pata picha 35 za mazishi ya Bi Shakila kuanzia nyumbani kwake hadi makaburini.
 Mwili wa Shakila ukiingwa ndani ya nyumba yake baada ya kuwasili kutoka hospitali ya Lugalo
 Banana Zorro akiwa na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
 Sehemu ya waombolezaji
 sehemu nyingine ya waombolezaji
 Simanzi ilitawala kwa wanandugu
 Kutoka kushoto ni Feruzi Juma mmoja wa viongozi wa kundi la Ogopa Kopa, mwigizaji Seif Mbembe na Said Mdoe 
 Kushoto ni Mwanne Othman mtangazaji wa East Africa Radio na mwimbaji mkongwe Sabah Muchacho
  Kushoto ni Hawa Hassan mtangazaji wa Capital Radio na ITV
 Katibu wa muda wa chama cha taarab Siza Mazongele
 Said Fella akisaini kitabu cha maombolezo
 Katikati ni mama mzazi wa Bi Shakila akiwasili msibani kutoka Morogoro anakoishi
 Mwimbaji mkongwe wa taarab Ally Star (katikati) akisalimiana na Mheshimiwa Nape
 Msafara wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ukiwasili msibani
 Mama Samia akiwasili msibani
 Mama Samia akisaini kitabu cha maombolezo
  Mama Samia akisalimiana na wafiwa
 Huzuni ilitawala nyuso za watu wengi
 Mheshimiwa Nape akitoa salam za pole kwa niaba ya serikali
 Mtoto wa marehemu akitoa salamu za familia
 Sala ya mwisho kwa marehemu
 Safari ya kuelekea makaburini
 Msafara wa makaburini ukiendelea
 Mkurugenzi wa Five Star Ally akiwasili makaburini
 Umati wa watu ukishiriki mazishi ya Bi Shakila
 Rais msataafu Jakaya Kikwete akishiriki mazishi ya Bi Shakila
 Mheshimiwa Nape na Kikwete makaburini
 Kikwete akishiriki mazishi kwa vitendo
 Umati ulikuwa mkubwa sana
 Mkurugenzi wa Babloom Seif Kisauji
 Kikwete akisalimiana na watoto makaburini baada ya mazishi
 Kikwete akiwa nyumbani kwa Bi Shakila baada ya mazishi
Rais mstaafu akisaini kitabu cha maombolezo

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *