RAPAHEL VARANE AFICHUA SIRI ILIYOMBAKIZA REAL MADRID


Raphael Varane says the presence of Zinedine Zidane convinced him to stay at Real Madrid

BEKI Raphael Varane amefunguka akisema kuwa ujio wa Zinedine Zidane ndicho kitu ambacho kilimfanya abaki Real Madrid.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa alikuwa akihusishwa kwenda kujiunga na Manchester United baada ya Jose Mourinho kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford.

Hata hivyo, Varane amekataa kuondoka katika klabu hiyo ya Santiago Bernabeu akisema anachokitaka ni kufanya vizuri zaidi akiwa na klabu hiyo ya jijini Madrid.

“Real Madrid ni mahali pazuri kwangu mimi kuendelea kufanya kazi,” Varane aliwaambia waandishi wa habari.

“Nilifanya uamuzi mzuri kubaki Madrid, ninaiamini klabu na ninamwamini kocha. Nimeshazungumza nae mambo mengi na ananiamini. Ujio wa Zidane ndicho kitu ambacho kilinifanya nibaki,” aliongeza staa huyo.

No comments