SALEHE PAKILA MPIGA SOLO WA JAHAZI KOLOMBWE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA FUSO


MPIGA gitaa la solo wa Jahazi Kolombwe Modern Taarab, Salehe Pakila (pichani juu) amefariki dunia kwa ajali mbaya ya kugongwa na Fuso usiku wa kuamkia leo.

Msanii huyo aliyekuwa akijulikana zaidi kama Pakila Solo aligongwa na Fuso maeneo ya Temeke Veterinary jijini Dar es Salaam jirani na kituo cha mafuta cha Oil Com.

Taarifa za uhakika kutoka kwa uongozi wa Kolombwe zimeiambia Saluti5 kuwa Pakila aliyekuwa anatokea kazini alipasuka kichwa na kufariki papo hapo.
INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJIOON

No comments