Habari

SCHWEINSTEIGER ASEMA ANA DENI MANCHESTER UNITED …adai hana tatizo na Mourinho

on

Bastian Schweinsteiger ameweka wazi kuwa hana tatizo na Jose Mourinho lakini bado anataka kuitumikia Manchester United.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, atacheza mchezo wake wa mwisho wa kimataifa Jumatano usiku, pale nchi yake ya Ujerumani itakapomenyana na Finland.
Schweinsteiger amesema bado anajihisi mwenye deni Manchester United ingawa aliweka wazi kuwa soka la Marekani linaweza kuwa chaguo lake lijalo.

SCHWEINSTEIGER NDANI YA MAN UNITED KWENYE PREMIER LEAGUE

Mechi alizocheza: 13 (5 akitokea benchi)
Magoli: 1
Mashuti makini: aslimia 33 
Nafasi alizotengeneza: 8
Pasi za uhakika: asilimia 85 
“Hakika ndoto yangu ni kuichezea Manchester United na kuisaidia kufikia malengo yao,” alisema Schweinsteiger kwenye mkutano na waandishi wa habari kueleka mchezo huo wa Ujerumani na Finland.
“Ni kweli tulikuwa na maongezi na sina tatizo lolote na Jose Mournho. Tulifanya maongezi mazuri, akanieleza mtazamo wake, lakini mimi pia najua nini ninachotaka.
“Tunapaswa kusubiri na kuona nini kitakachotokea kati ya mwezi Septemba na Oktoba”.
Wiki kadhaa nyuma Mourinho ameweka wazi kuwa kiungo huyo hana nafasi Manchester United ambapo alimtaka atafute nyingine.
Schweinsteiger was speaking at a press conference before Wednesday's game with Finland
Schweinsteiger bado anataka kubaki United
Mourinho has told Schweinsteiger that he is unlikely to play if he stays at Old Trafford
Mourinho alimwambia Schweinsteiger hana nafasi Old Trafford.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *