TWANGA PEPETA KUFUNGUA UKUMBI MPYA WA SAVOY – BUZA LEO USIKU


Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” leo usiku itakuwa na onyesho maalum la ufunguzi wa ‘kiwanja’ kipya cha burudani jijini Dar es Salam.

‘Kiwanja’ hicho kinakwenda kwa jina la Savoy Pub ambacho kiko pande za Yombo Buza Kanisani.

Mkurugenzi wa Savoy Pub, Mr Elkana ameiambia Saluti5 kuwa ametoa ofa kwa wapenzi wote watakaofikia leo kwenye ukumbi wake kwa kuwalipia kiingilio, hivyo kila shabiki ataingia bure.

“Ni ukumbi mzuri, mkubwa na wenye mandhari ya kuvutia, naomba mashabiki wajitokeze kwa wingi waje kushuhudia eneo jipya la kujirusha, wasihofu kuhusu kiingilio, Savoy tumeshagharamia kila kitu,” alisema Elkana.

Twanga Pepeta inatarajiwa kupambwa na nyota wake wote wakiwemo Ally Chocky, Khalid Chokoraa, Luizer Mbutu, Ferguson, Kalala Jr, Rogart Hegga na Haji BSS.

Onyesho hilo linatarajiwa kuanza saa 12 jioni na kuendelea hadi usiku mnene.

No comments