Habari

WAYNE ROONEY AAMBIWA HASTAHILI KUPATA NAMBA MAN UNITED …kisa? uzito ummemzidi

on

England striker Rooney has been at Old Trafford 12 years and must now fight for his place
Wayne Rooney amekuwa mzito na hana kasi uwanjani hivyo hastahili kupata namba kwenye kikosi cha Manchester United.
Hayo ni maoni ya beki wa zamani wa Engaland, Paul Parker ambaye alishinda mataji mawili ya Premier League akiwa na Manchester United baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 2 mwaka 1991 akitokea QPR. 
Rooney alifunga bao moja katika ushindi wa 3-1 kwenye Premier League dhidi ya Bournemouth Jumapili iliyopita, lakini Parker anasema mshambuliaji huyo wa England hayuko fiti kimwili kiasi cha kustahili kuwepo kwenye kikosi cha kikosi cha kwanza cha United.
Wayne Rooney scored at Bournemouth but Paul Parker was decidedly unimpressed
Licha ya Wayne Rooney kufunga dhidi ya Bournemouth lakini Paul Parker hakuvutiwa naye
Parker, (grounded) in action during the 1994 FA Cup final, moved to United in 1991
Parker, (aliyelala chini) akichezea United mwaka 1994 kwenye fainali ya FA Cup 
Rooney featured for 89 minutes at Bournemouth, playing behind striker Zlatan Ibrahimovic
Rooney alicheza kwa dakika 89 kwenye mchezo dhidi ya Bournemouth, akicheza nyuma ya Zlatan Ibrahimovic

Parker, akiongea na 888.com, akachambua ujio wa Paul Pobga aliyesajiliwa na Manchester United kwa pauni milioni 100.
“Kukiwa na Paul Pobga unashangaa, pale unapoangalia staili yake ya uchezaji alivyokuwa nayo Juventus, je anaweza akacheza kwa mfumo ule ndani ya Manchester United?,” anahoji Parker.
“Kama atacheza nyuma ya  Ibrahimovic hiyo itamweka Wayne Rooney mashakani lakini hapo hapo ukumbuke kuwa Rooney anatakiwa kucheza – sio kwa sababu anastahili kupata namba, hapana hastahili kucheza kwa sasa lakini wanalazimika tu kumchezesha. Hiyo ni hali ngumu sana”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *